Kila tarehe 8Machi..tunasherehekea siku ya wanawake duniani...
Kwa nchi zetu za Afrika kutokana na tamaduni zetu mwanamke amekuwa akitazamwa kama kiumbe duni,dhaifu,kinyonge kisicho na sauti..
Kwa hapa Tanzania tumeshuhudia wanawake wakitendewa vitendo vya kikatili kama kubakwa na kupigwa mpaka hata wengine kuuawa..
Lakini leo tunapoiadhimisha siku hii kama wanawake wa kiTanzania tuamini kuwa tunaweza kufanya jambo lolote na likafanikiwa pale tu tutakapoamua..Tunayo mifano mingi ya baadhi ya wanawake wenzetu wanaoijituma kwenye masuala mengi na kufanikiwa.
Kama uko shule ni wakati wako kutumia fursa uliyonayo kwa juhudi mpaka kufikia lengo lako..
Uko kazini fanya majukumu yako bila woga au kuona hiki ni cha kiume mimi kama binti/mwanamke siwezi..
Kuzaliwa mwanamke ni zawadi..usikubali kukata tamaa na hata kuona huwezi au hufai..
pengine hali ngumu ya maisha imekupelekea ufanye njia hatarishi za shortcuts ili uvuke..
Hiyo si sahihi.bado fursa ziko wazi tafuta watu unaowaamini washirikishe yale unayotaka kufanya..Watakupa mwongozo..
Happy women's day...!
Mwanamke...
Jipende...
Jikubali...
Jiamini..
Timiza ndoto zako..
kisses to all ladies..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment