Leo natamani tupate mashairi ya wimbo wa BALEKA ulio kwenye album ya 17 ya Joyous Celebration na kuimbwa na mwanamama Nobathembu Mabeka..
Baleka kwa kiswahili inamaanisha KIMBIA.
na kuna maeneo mengi ambayo umeyataja mno.
√ wewe binti uliyeko shule na kuna sugar daddy anayekupa mahitaji yako..unapaswa kukimbia kwa miguu yako miwili..
√wewe mkristo mbona mnamsengenya mwenzenu kwani hamjui madhara yaake..?
√wewe mjane mbona kuna mme wa mtu kutwa kucha anakuja kwako na kulalamika mkewe hampikii..mbona hujiulizi kwa nini anakuja kwako?.
√wewe mkaka kuna binti anakupigiaga simu kila saa nane alfajiri..hushituki tu anataka nini kwako?
Baleka..baleka
Baleka.ngenyawo zombili(kimbia na miguu yako miwili)
Ukaendelea kusema kama wakristo kuna mambo hayataki maombi/kupiga magoti..yanahitaji mbioo..
Natumai ujumbe huu utakufaa kwenye bĂ adhi ya maeneo ya maisha yako..
Uwe na wiki ya mafanikio..
Mapendo tele kwenu..
Mungu anakupenda..nami pia nakuthamini..
No comments:
Post a Comment