Tuesday, March 4, 2014

Saratani ya shingo ya kizazi...

Ni muda mrefu hatujazungumzia mambo ya afya..
Tukiwa na siku chache kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani hebu tujifunze hili..
        Saratani hii ya shingo ya uzazi husababishwa na kirusi kiitwacho Human Papilloma Virus..

Na maambukizi yake huchangiwa saana na:

 √kujamiiana.
√Kuwepo na maambukizi katika uke kama vile zinaa.
√Kujiingiza vidole ukeni..haswa wakati wa kujiswafi 
√kuvuta sigara.
√Ngono ya mapema na haswa wale wanaofanya na wapenzi wengi..
√Kujamiiana na mwanaume asiyetahiriwa.

Dalili za tatizo hili ni:
#**Kutokwa damu ambayo si ya kawaida ukeni na wakati wa hedhi.
#**Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa/kujamiiana.
#**Maumivu wakati wa tendo la ndoa..

Umri wa kupata maambukizi haya ni kuanzia miaka 15-44..Lakini kwa usalama waweza tembelea hospitali yoyote na kufanya vipimo..

No comments:

Post a Comment