Monday, March 3, 2014

Binti Inuka....mafanikio ni haki yetu

Ukifungua kila chombo cha mambo ya burudani kwa muda sasa na hata kwenye masuala ya urembo..huwezi kupita bila kumuona binti wa Kenya..tena m-Luo..LUPITA NYONG'O..

*Alizaliwa huko Mexico 1.3.1983na Profesa Amondi ambaye alikuwa ni mhadhiri wa masuala ya sayansi ya siasa huko Mexico..
 *Mama yake pia ni Managing director wa African Cancer foundation..
Dada huyu ambaye ni msomi na ni mwigizaji na Music video director amejizolea umaarufu hasa kwenye filam ya Steve McQueen's ya 12Years a Slave.ambapo amejitwalia tuzo lukuki..

Lupita akiwa bado hajawa maarufu alipata shida sana kutokana na rangi ya ngozi yake..ilimpa shida na kumkosesha ujasiri..lakini alitiwa moyo alipomuona mwanamitindo Alek Wek kutoka Sudani kusini.Akaamini kufanikiwa inawezekana na kikwazo si rangi ya ngozi yake..
katika hali iliyoshangaza wengi ni katika red carpet walipokuwa yeye na familia yake baba yake aliongoza maombi ndipo wakaingia ndani na bintiye akatwaaa tuzo hiyo ya Best Supporting Actress kwenye movie ya 12 years a slave alioigiza kama Patsey..
          Binti mwenzangu kuna wale ambao mmepitia manyanyaso ya kihisia kutokana na rangi ya ngozi yako..Dont hate your skin colour..cherish your beauty and even your body..If someone is not comfortable with your  skin and appearance that is their problem not yours..simamia ndoto zako na Mungu yuko nyuma yako kukuwezesha..
Lupita ameweza na sisi tunaweza..

Kuelekea siku ya wanawake duniani..tujipende ...tujiamini na tujipende....
Muahhh to you all ladies

No comments:

Post a Comment