kama nilivyoahidi facebook..ningependa tujifunze hapa jambo ambalo unalijua au hulijui lakini ni la msingi..
Jinsi ya kuwa mwanamke mwenye ushawishi(influence) ambapo watoto wako ,mume wako huko baadaye na jamii itanufaika nawe..pale wanapokutazama wanatiwa moyo,wanajifunza na zaidi kupiga hatua fulani.
Hii ni moja ya zawadi tuliyotunukiwa wanawake na Mungu ikitumiwa vizuri huzaa mema na ikitumiwa vibaya huleta maafa makubwa.
kwenye utafiti uliofanywa juu ya mambk ya Mungu ambapo watu wa jinsia zote waliulizwa "whi has a positive influence on religious basis"? majibu yalikuwa my mother na waliooa walijibu my wife
kwa upande wa sayansi ya jamii tunasema mwenye jukumu la kuhakikisha anamfunza mtoto maadili na utaratibu wote kwenye jamii ni MAMA ndio maana mtoto mwenye tabia mbaya akipatikana watu huulizana mamake kamleaje huyu?(Mithali 27:11)
Au kwa mwanaume aliye mtanashati kastaarabika watu husifia mume wa fulani bwana kwakweli katunzwa katunzika(Mithali 31:23)
Sasa unapoafikiana na huyoo kijana wa watu kuwa tuyaanze mahusiano baadaye uchumba mpaka ndoa lazima uwe na akili ya ziada kuwa una jukumu la ushawishi chanya na utakaomfanya akue zaidi kwenye ndoto zake na hata maisha yake yawe ya ustawi..
ninapata maoni ya vijana wa kiume kwamba kwao kutumia pesa si tatizo hasa wanapogundua msichana aliye nae anapenda kujiachia..sasa incase unapata mwenye pesa hizo use ur power of influence kumuelekeza matumizi sahihi ya pesa na si kuzitapanya wee..
SIFA ZA mwanamke mwenye influence
√ni muombaji na si kuomba tu bali amejaa imani kuwa chochote anachotaka kitokee kwa watoto wake,mmewe na yeye binafsi lazima kiwe..kwa kuwa ni ngumu kufikia malengo pasi na kumshirikisha Mungu
√ni mtii...
√ana upendo-hakuna atakayekubali kushawishiwa na mtu asiye na upendo...upendo ni kujitoa wakati wote tukumbuke upendo wa mama yake Musa alivyo risk maisha yake na kumtengenezea mwanae kisafina asiuwawe na farao..yule mama pia aliyekwenda kudai mtoto wake kwa mfalme suleiman nk.
Sasa hakikisha unajua majukumu na nguvu uliyonayo kwenye uhusiano uliopo..kama
1.kuwa mshauri-hapa biblia inainsist Godly counsel na kama mwanamke unayo hiyo neema ya kushauri hivyo msihi Mungu akupe hekima kila leo ili utoe shauri njema
2.uwe wa kutia moyo.-pale anapofanya mazuri au hata kukata tamaa muombee na muonyeshe bado anayo nafasi ya kufanya mazuri..
3.uwe wa kujenga-kuwa mbunifu shirikisha mawazo yako kwake kwamba nilifikiri tufanye hivi au kwenye hilo ulilo nalo lifanye hivi sio kila mara wewe ni kubomoa tu na kukatisha tamaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment