kwa tulio marafiki facebook niliahidi weekend tutakuwa inspired na mwanadada Faraja Kotta Nyalandu...
Nilipata bahati ya kumuona akizungumza kwenye kongamano la mabinti la Ladies of destiny mwaka jana lililoandaliwa na Rose Mushi.
Faraja ni dada msomi na aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2004..
Kuna vitu vikubwa vitatu vya kujifunza kwake.
√akiwa sekondari aliwahi kuandika insha iliyopelekwa ikulu kipindi cha rais Mkapa na kumpa fursa ya kwenda umoja wa mataifa pamoja na fedha za zawadi ambazo anasema alizitumia kununua viwanja na mashamba...Si mara yake ya kwanza kung'aa hivi akiwa shule kwani akiwa kidato cha sita alikuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora..
√Faraja ameanzisha tovuti ya www.shuledirect.co.tz ambayo imelenga kuwapa syllubus wanafunzi pamojana mitihani ya majaribio itakayo wasukuma kwente ufaulu mzuri nawao kufikia mafanikio kitaaluma.
√Wiki hii pia amezindua kitabu chake chenye kuelezea mbinu za kutosha kumfanya mwanafunzi afaulu mitihani..
Lengo la kumuweka dada huyu ambaye ni mke pia waWaziri Nyalandu na mama wa watoto wawili ni jinsi anavyopangilia mambo yake,tumeona hapo kwenye masuala ya pesa kuwa si kila pesa ni ya kuchezea la hasha zipangie jambo la msingi na maendeleo la kukusaidia..Na anaonyesha ni mpambanaji haswaa...
Amekuwa ni mfano pia kwetu kuwa ukiwa na ndoto inaweza kutimia wasichana wengi hatupendi kuthubutu sasa ni ngumu kufikia malengo ikiwa hatuchukui hatua...nikinukuu moja ya sentensi zake kwenye kongamano "napenda kuziamini idea zangu na kuziweka kwenye utekelezaji bila kuacha kumshirikisha Mungu kwa sababu yeye ndio kila kitu"...na tumeona ayafanyayoDada mwenzangu ni kipi unachowaza kufanya ??nilishauri sehemu fulani ikiwa wewe ni mpishi mzuri na kila mtu anavutika na upishi wako ni hakika kuwa kupitia hicho maisha yako yatabadiklika na utasaidia jamii pia..
•anza hapo hapo nyumbani ikitokea unapika act tovyour dream be as if una own your own catering and umealikwa sehemu kupika who knows yawezekana watakaokula siku hiyo wakawa ni wageni na wakakupa fursa upike kwenye shetehe majumbani mwao na huko ukakutana na wengine..
waweza kuwa na chochote jiamini katika hicho halafu chukua hatua..si kila kitu kinahitaji pesa wakati mwingine piga hatua watu wakuone waje wakuuunge mkono...
We ladies can...
identify what you want to do ...
tenga muda kupata taarifa juu ya hicho unachotaka kufanya...ingia uwanjani kwenye utekelezaji..
AMUA na UWEZE...
No comments:
Post a Comment