Sunday, December 1, 2013

unafanyaje ndoto yako inapotoka100km to 50 km

Maisha yana kupanda na kushuka,maisha hayakamiliki mpaka nyakati zote zimekuwa bayana kwani zipo nyakati za machungu na furaha,mara nyingi nyakati ngumu hufunua mambo mengi ambayo kipindi ukiwa na nguvu zako huwezi kuyaona.Hukufanya uwe mvumilivu,jasiri kwa wengine huwafanya kujitambua wana tabia za aina gani..

Hakuna mtu anayeishi pasipo mipango au ndoto kwenye maisha.Si kila unachopanga kitatimia kuna ambavyo vitakwama ndiyo maana unakuta ulipanga mipango ya km 100 ghafla maisha yanakutikisa zinabaki 50 kms.ni sawa na mtu aliyekata tiketi ya kwenda morogoro na Abood anafika stand anaambiwa Abood zoteee zimeondoka Lakini kuna Hood au Islam muda huu uliofika je?ungependa kuondoka na basi lipi.Hapa ishu ni kufika Morogoro kwa hiyo si busara kususia hata ulichokikuta eti kwa sababu halikuwa chaguo lako..

***Leo tutajifunza nini ufanye mipango yako mikubwa inapobaki robo,labda ulitamani  mwendo wa mafanikio ya km 100 ukajikuta zipo km 50.********


π√kubali kwamba ulikuwa na 100 na sasa zimebaki 50.
π√Mshukuru Mungu kwa hizo 50 zilizopo.
π√Amua kutoka ndani(desire from heart)kwamba kupitia hizo 50 zilizopo mafanikio na ndoto zako lazima zitimie.
π√Sahau 50zilizopotea ongezea bidii kwenye kile ulicho nacho.mfn: kama ndio yule msafiri achana na kumbukumbu za Abood,tengeza mazingira ya safari yako na Islam/Hood kufika unakotaka.

Usijikatishe tamaa kwa ulichopoteza kizingatie kile ulichonacho mkononi bado ,,hicho ndicho cha msingi.
°•kwani unapo download kitu unakuwa na hali gani???si unakuwa attention mpaka kitu kitokee.Au kikiandika LOADING si unasubiria!! vivyo hivyo na baadhi ya mambo kwenye maisha yanataka hiyo nidhamu ya (loading/downloading) apart from that utabaki kunung'unika tu.


No comments:

Post a Comment