kila binadamu mwenye sifa saba za viumbe hai,anapokutwa na jambo lenye kuumiza huumia na huchukua muda sana kusamehe na kusahau.
Lisa akiwa binti mdogo kipenzi cha babayake aliumia sana siku alipoamka na kukuta babaye aliyempenda sana amefariki,hakukaa sana mama yao aliolewa tena,maisha yao na baba mpya hayakuwa marahisi kwani yalijaa manyanyaso na kukosolewa kusikoisha,la kuogofya zaidi ikiwa ni uso wa babaye mpya uliokuwa una tundu kubwa sana lilishonwa na kuacha uso ukiwa wa kutisha..siku moja Lisa alikaa chini akawaza juu ya babaye huyu na jinsi gani amsamehe,ndipo alipomba wazungumze ili kuondoa tofauti zao.kabla Lisa hajazungumza babaye huyo alijieleza kuwa wakati akiwa mdogo kama Lisa babae wa kambo alitaka kumuua na aliporusha risasi ilimpata na kumfua sehemu hiyo ya uso,ingawa aliumia aliamua kumsamehe babae na kuendelea na maisha yake...Baada ya hadithi hii Lisa ilimbadili sana na akaamua kusamehe na akadema ikiwa nilie na kinyongo nae aliwahi tendewa unyama nakusamehe na mimi naweza pia....
kusamehe ni nini???
kusamehe ni tendo la kiakili na kiroho la kuamua kwa hiari kuachilia chuki kisasi,kinyongo juu ya mtu..
na huwa haimaanishi tumeliridhia/likubali jambo mtu alilofanya kuonekana si kosa,la hasha mara nyingi tunalenga KUJIWEKA HURU na kujiondoa kwenye kubeba mzigo wa mambo ya kale...
kusamehe siku zote hutuhusu sisi binafsi kwani hutuponya majeraha yetu na kutupa fursa ya kuendelea mbele na maisha yetu.
√hutupa fursa pia ya kujifunza kwa njia chanya kupitia maumivu hayo na kutufanya tuwe bora zaidi kimtazamo na kifikra.
√kusamehe huchukua muda kidogo lakini faida zake ni kubwa sana...hukupa uhuru wa kufurahia maisha yako na fursa ya kuwapenda wengine..
√kusamehe hufungua baraka pia....
Tunapomaliza mwaka na hata kwenye maisha tunaumizwa,tunaumiaa sana lakini kusamehe ndiyo suluhu ya yote..kuna mambo Mungu hawezi kukupa kwa sababu umejaza uchungu ndani na kisasi..
Yaachilie na amua kusamehe utaona furaha na baraka zikimiminika kwako.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment