Saturday, November 23, 2013

jifunze kupitia Kirk Franklin!!!


Kirk D
wayne Franklin si jina geni hasa kwa wapenzi wa gospel.
√amezaliwa tarehe 26.1.1969 huko Forth Worth Texas.
√ ni mwanamuziki,mwandishi na mtayarishaji wamuziki na vingine vingi.
√chombo cha muziki akipendacho ni PIANO na hukitawala sana akikipiga.
Kirk Franklini akiwa mtoto alitelekezwa na mama yake hivyo kuishi maisha ya mateso sana yaliyompelekea kuwa na matatizo mengi ya kinidhamu akiwa shule na hata kwenye jamii.
√mwaka 2005 akiwa kwenye kipindi cha The Oprah Winfrey Show alikiri hadharani kuwa alikuwa ni '"Pornography addict" na kitu kilichomsumbua kwa muda mrefu mpaka alipochukua hatua za kupata shauri za kikristo na yeye kuwa huru,jambo hili lilileta msuguano na mpenziwe ambae ni mkewe sasa maana walipoanza tu uchumba Kirk alieleza udhaifu wake na wakati mwingine alileta video hizo za ngono wazitizame pamoja ndipo mrembo huyo alipompa No kubwa si kumkataa bali kukataa video hizo na kumsihi waandamane pamoja apewe msaada wa kupona tatizo hilo,na akiwa kwa Oprah aliambatana na mkewe huyo kipenzi.

•√lengo la makala hii ni kuchambua vitu vitatu vya kutusaidia mimi na wewe.
1.background zetu hazina sauti kubwa  kutuzuia kuishi vile Mungu ametaka nakufika kule unatakiwa uwe,Kirk alikuwa na background ngumu cz kukosa malezi ya mama si mtihani mdogo huo,je mimi na wewe ni hali gani zimetukumbatia uyatima,maisha magumu,kukosa pesa au nini?ambacho ukikiangalia unaona mmh na hali hii nitaweza kweli mimi?kwa nini usiweze umewahi jua background za kina Joyce Meyer,Oprah,Mengi,Bill gates,Leonel mess na wengineo nao walikabili michongoma na maumivu walioamua kuyapuuza na kutimiza ndoto zao.Leo hii ulimwengu wote unamtaja Kirk na kuimba nyimbo zake,what if na yeye angejikumbatia na uyatima wake huo si angeupunja ulimwengu baraka tele zilizomo kwenye nyimbo zake.

2. wale wenye addiction za kitu chochote kiwe pornography, masturbation,au chochote jua kwamba suluhisho lipo na ni rahisi tu.Ile dhamira ya ndani ya ukiri  wa tatizo lako na uradhi wa kuacha ndio ukombozi wako.hujachelewa neema ya Mungu ipo kukusaidia jijenge kwenye maombi na kulisoma neno la Mungu kutakusaidia pia.umemuona Kirk pia alichukua hatua akatibika na maisha yanaendelea hiyo imekua history keake sana.you can overcome too.

3.wale wenye relationships kuna la kujifunza pia hapa,ni vizuri ukiujua udhaifu wa mwenzio ukamsaidia kwa upendo.a problem shared is a problem solved,be open to each other ili msaidiane as how the couple did and here is a very strong foundation as you will all know each other best and pray to lift one another.Because love covers.

#ni maombi yangu ufanikiwe sana,na kila kinachozuia mpenyo kuzifikia ndoto zako kikuachie katika jina la Yesu.upokee nguvu na uweza kufanya ulilopanga katika jina la Yesu.Amen



No comments:

Post a Comment