Thursday, November 14, 2013

Insecurity problems

unawajua watu wenye tatizo la insecurity Hawa ni watu wasiojikubali au kuridhika jinsi walivvyo au walivyokuwa Navyo.

viashiria vya wenye insecurity:
#daima wakiona MTU ana kitu wasichoweza kuwa nacho au kukifanya huwa defensive kupitia udhaifu wao kwa kuwakosoa wenzao au kuwavunja moyo ukibaini utagundua hayo maoni yana chuki au yeye hana ubavu wa kufanya jamboulilofanya au kama ni nguo angeivaa yeye isingemtoa chicha kama wewe,ili wote mshiriki udhaifu wake anakupa hayo maoni yakurudishe nyuma.Nakumbuka enzi hizooo nilikua na idea zangu kila nikiwa na huyo rafiki lazima anambie mweee kufanya hayo ngojea miaka 100 ndio utatimiza, nikikuangalia sioni kama utafika sehemu. ila siku nikajifunza kupitia story zetu nikaangalia yeye anayowaza nikaona hana idea yoyote aliowahi nipa so haoni Kile Mimi nakiona na anataka niwe kama yeye ikabidi nijifunze kusimamia ndoto zangu mwenyewe.


#utawagundua kwenye kauli Zao,badala ya kusifia,kutia moyo wao hukosoa au hujitahidi kurekebisha,kama ni namna umevaa atakuambia umependeza saw a LAKINI ungefanya........
 au kuimba umeimba ILA ungepandisha key kidunchu....


#kama Uko nao kwenye mahusiano ya kimapenzi huwa ni wanyanyasaji na hutumia nguvu kuficha udhaifu wao kwa kuwanyanyasa kihisia wapenzi wao(emotional abuse)ie:kuwakosoa kimaumbile mfano,rangi ya ngozi ysko bwana nyeusiiii,unanenepeana ovyoo,kama umedhindwa kusuka hizo nywele si ukate tu kwani mwenzio nanii humuoni anavyojiweka soap soap.

Jinsi rahisi ya kuishi na watu Hawa ni kusimamia kidete mawazo na mipango yako.ukishawabaini we we songs mbele endelea kuwaombea,ukiwapa nafasi utajikuta kama ulikuwa mweusi umejichubua,ulikua una talent zako unaacha kumbe hilo ni tatizo LA kisaikolojia na linatibika pale mhusika ana pojigundua na kutafuta tiba.

√nothing is impossible to a daring heart I pray that ushinde vipingamizi vote unavyopitia au ulivyopitia hata kama uliambiwa we we ni mbaya endelea kujitunza nakujipenda yupo atakayekupenda hivyo ulivyo,na waliokumbia huwezi wapuuze simamia unachoamini na utafika ng'ambo.
love y'all

No comments:

Post a Comment