Katika maisha ya kawaida usafi wa mwili unahusika sana,kama vile unavyoona umhimu kula chakula jua pia na mwili unahusika sana kuutunza usipate magonjwa na pia usiwe kero kwa wanao kuzunguka.Tutaangalia leo kuhusiana na kutatua tatizo la jasho au kikwapa,,mwili unapofanya kazi au hata wengine ni maumbile tu hutokwa na jasho sana, si vibaya...lakini lipo ambalo huwa kero na hata wengine huacha alama ya njano kwenye nguo zao...Jasho lenye kutoa harufu au shombo linatibika,,,.
jasho/kikwapa linatibika kwa njia za asili hasa kwa kutuma limao au ndimu kuokoa gharama za marashi ambazo ni njia za kisasa ambazo si kila mtu anaweza kuzimudu.Lakini limao na ndimu unaweza kununua au kulichuma nyumbani kwako....
Unaweza kulitumia limao au ndimu kama tiba ya kikwapa,zoezi hili hunoga zaidi muda ule unaojiandaa kwenda kuoga.
HATUA!!!!!!!
- kata vipande viwili na ondoa mbegu, kipande kimoja kisugulie kwenye kwapa la kulia na kingine kwapa la kushoto.
- kaa kwa muda wa dakika kumi hadi ishirini wakati unajiandaa kwenda kuoga.
- baada ya dakika hizo kutosha waweza koga sasa huku ukipaka eneo tajwa sabuni ya kutosha na kupasugua na kitambaa laini....
- Kama una haraka sana unaweza kupaka kama dodorant yako, focus ikiwa ni kukata ile shombo ya jasho.
No comments:
Post a Comment