Kwanini unataka/kuwaza kujiua?
Kwanini unakata tamaa?
Unapochagua Kimoja Kati ya hivi viwili hututendei na hujitendei haki,unatupunja hasa maana kuna vingi Mungu ameweka ndani yako ambavyo hatuwezi kuvipata popote hata tuzunguke Mabara yote ya dunia hii ni wewe tu unayeweza kufanya hayo,hata Kama wewe unayaona manyonge na yasiyo na maana kuna mtu anayahitaji mno.
Unapoamua kutaka kuondoka kwa kujiua nani unafikiri ataziba pengo lako?hizo haiba zako Kama ucheshi,utani,na hata vipaji vyako tutavipata wapi?
Nani amekudanganya kujiua/kukata tamaa ndio suluhu ya mambo hayo yanayokusonga?
Mitihani ya maisha humpata kila mmoja..Kikubwa ni kutokukata tamaa..kupambana..kujikubali. .kujithamini na kujiona mtu mwenye mchango katika sayari hii bila kuangalia udogo/ukubwa wa hadhira au mazingira yaliyokuzunguka..
Unapendwa...
Wewe u wa thamani. .
Songa mbele..
No comments:
Post a Comment