Wengi tunamwita Mungu baba,hakuna mzazi anayependa kumuona mtoto wake akiumia nakuteseka,na leo likumbuke hili kuwa hilo nalo litapita na itakuwa ushuhuda tu.
√hilo unalopitia lisivuruge ratiba nyingine za maisha yako,maana mwingine akiwa na gumu anaacha kula,kupendeza au hata kujichanganya na wenzie,mpendwa wangu usiiname moyo kwa kiwango hicho
(1Korintho 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi,isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu;ila Mungu ni mwaminifu ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo;lakini pamoja na lil jaribu atafanya na mlango wa kutokea,ili mweze kustahimili).
√neno hili likujenge katika hali yoyote unayopitia kwamba hilo si jambo geni katika listi ya magumu ya dunia hii wapo waliopitia kipindi kama chako na wakavuka maana anayetuvusha ni Mungu na si mbinu au ujanja wetu wa kibinadamu.Ngoja nikupe ushuhuda wangu
#tarehe 16.12.2012 nilipata ajali mbaya sana ya pikipiki ambayo nusura ichukue maisha yangu iliniachia picha ngumu sana kichwani mwangu na zaidi ilibadilisha ratiba nzima ya maisha yangu na kunifanya nianze upya kabisaaa!nilitiwa moyo na familia na marafiki lakini ilikuwa ngumu kukubali hali mpaka siku moja nilipoamua kumwambia Mungu japo kwa machozi kwamba nakushukuru kwa hili na lile naomba nipe mafundisho sahihi yatakayouponya moyo wangu na kunipa nguvu za kutetea ndoto zangu na kukutumikia wewe,napenda sana kusoma online nikiwa nasearch baadhi ya blog nilikutana na blogu ya Samwel Sasali na moja ya post niliyosoma ilibeba story ya rafiki yake aliyepata ajali mbaya sana ya gari na alitoka hai when I saw the picture of that accident na jinsi yule kaka anavyomtukuza Mungu na kuendelea na maisha yake so focused and happy,i cried loud to my parents and confessed so many things about myself kwamba kama yule kaka alilivuka lile na anaishi ndoto zake what about me?nilijiinua nakusonga mbele where I have done so many things and am stilll doing for GODs glory..
picha hii ni ya Prosper Mwakitalima rafiki wa Samuel Sasali aliyenusurika kifo baada ya ajali hii mbaya. |
√nakutia moyo tena haijalishi ni gumu gani,maisha lazima yaendelee,
*We fall 7 times and standup 8.
*God brings men into deep water not to drawn them but to cleanse them.
*Get going,move forward,aim high,change your attitude and gain some altitude.
You will rise again...ninakuombea utavuka hilo na utakuwa ushuhuda...
#kula vizuri,pendeza sana,jichanganye,changamka,mtegemee Mungu..kama wengine wameshinda ni jawabu tosha nawe kuwa Ni MSHINDI wa yote unayopitia.
No comments:
Post a Comment