Wednesday, October 23, 2013

hakikisha unajifunza jambo katika kila gumu upitialo!!!!!!


Maisha yamejaa mitihani ya kila aina na kila linapoisha hili huzaliwa jingine.Lakini kuwepo kwa matatizo hakutufanyi kushindwa kufikia ndoto zetu na baraka ambazo MUNGU  ameziambatanisha na maisha yetu,uzuri wa mtihani huwa ni jambo la muda tu si la milele,, lakini nini unafanya wakati wa tatizo lako na UMEJIFUNZA NINI ndilo jambo la msingi la kulitizama.Matatizo ni sehemu ya maisha kama vile kulivyo na majira mbalimbali katika maisha wakati wa jua,mvua n.k,majira haya hutumika tofautitofauti,kwa mfano: mvua hunyesha ili kuhakikisha inazalisha na kitu kinapatikana,jua husaidia kukausha kile kilichozalishwa kwa matumizi maalumu.Ukitazama safari ya wana wa Israel jangawani ilikuwa yenye kiu,njaa na mateso makubwa lakini mwisho wa siku walifika walikopaswa kwenda sometimes nilijiuliza ikiwa MUNGU aliweza kuwapa waliyotaka kwanini asingetumia ile njia ya mkato na ilikuwepo???nikagundua kuna mambo MUNGU hutaka tujifunze ili tuchangamke na kukua na tukitoka pale tunaweza kusuluhisha baaadhi ya mambo bila kilio tena.
Hakikisha unajifunza kitu badala ya kulalamika au kutafuta nani chanzo cha tatizo
  • chukua tatizo lako,kaa chini lichunguze nini kilipeleka jambo hilo kutokea na kama limejirudia kwanini??
  • Ikiwa unamwamini MUNGU omba akufundishe nini haswa unapaswa kujifunza katika tatizo hilo na baada ya ufumbuzi ni maisha gani unapaswa kuishi baada ya solution kupatikana...
  • Amua kutoka ndani kuwa umejifunza,UTAJIFUNZA NA KUTENDEA KAZI FUNZO HILO!!
    Wakati fulani nilipitia changamoto ngumu sana nikajiambia mwenyewe kulia hakutakuwa suluhu lazima nijipange kulikabili tatizo na kulishinda na kuhakikisha nimejifunza ili nisilie tena,nilipoamua hivyo nikapata amani,nikasoma maneno ya MUNGU na kutafuta bogu za kikristo zilizoniimarisha sana na kuniacha nimesogea na kupiga hatua kubwa sana katika maisha yangu,,
Usilie tena,usijilaumu hilo unalopitia litakwisha lakini hakikisha unajifunza kitu kitakachobadili maisha yako!!!nakuombea uvuke salama katika gumu hilo na pia ujifunze kwa usahihi ili uishi maisha ya ushindi na mafanikio....

1 comment:

  1. Waoh nmejifunza kitu.Asante sana na Mungu akubariki.

    ReplyDelete